KIFO CHA KUSISITIZA KATIKA CHUO KIKUU CHA JARAMOGI OGINGA ODINGA

Written by on May 12, 2026

Katika mji mtulivu wa bondo, giza nene lilitanda kufuatia tukio la kuhuzunisha lililokatiza ndoto za mwanafunzi mchanga wa chuo kikuu cha Jaramogi Oginga odinga cha Sayansi na Teknologia . Binti huyu aliyekua na matumaini yake kesho iliyo bora, alipatikana ameuawa kinyama ndani ya nyumba yake ya kukodisha nje ya chuo hicho. Habari hizi zilisambaa kama moto, zikiacha simanzi na hofu tele miongoni mwa wanafunzi wenzake na wakazi wa eneo hilo ambao hawakuamini ukatili huo. Siku ya tendo hilo, inadaiwa kuwa majirani walisikia mzozo mkali ukifuatiwa na ukimya wa kutisha lakini hakuna aliyejua kuwa maisha yanatoweka. Mwili wa mwendazake ulipatikana ukiwa na majeraha mabaya , ishara tosha ya mapambano ya mwisho ya kuokoa maisha yake. Polisi walifika eneo hilo la tukio na kulizingira, huku wakikusanya ushahidi wowote ambao ungewaelekeza kidole cha  lawama kwa mpenzi wake wa zamani.

Inasemekana ya kwamba mpenzi wake alishindwa kukubali mwisho wa uhusiano wao . Wivu za kijinga na hasira zilizodhibitiwa zilitajwa kuwa chanzo cha mauti hayo, jambo ambalo limekua ndonda  ndugu katika vyuo vikuu vingi nchini. Simulizi za marafiki wa karibu zilifichua kuwa binti huyo alikuwa akiishi kwa hofu kwa mda mrefu, akipokea vitisho vya mara kwa mara bila  kujua kifo kilikua kinamvizia mlangoni. Kufuatia mauaji hayo , wanafunzi  wa chuo kikuu cha Jaramogi Ogiga Odinga cha Sayansi na Teknolijia walifanya maandamano ya Amani wakitaka haki itendeke na usalama uimarishwe.

Wanafuzi hao wa chuo kikuu walibeba mabango yenye jumbe za kulaani mauaji ya wanawake, huku wakitoa wito kwa serikali na usimamizi wa chuo hicho kuchukua hatua madhubuti. Kilio chao kiliokuwa kimoja “Haki kwa wenzetu” kwani walihisi kuwa kifo chake hakikuwa tu pigo kwa familia , bali ni tishio kwa uhuru wa kila mwanafunzi wa kike.

Mshukiwa alitiwa mbaroni baada ya msako mkali wa polisi , akisubiri kufika mahakamani kujibu mashtaka ya mauwaji. Ingawa kukamatwa kwake kunatoa matumaini ya kupatikana kwa haki , pengo aliloacha binti huyo halitazibika kamwe. Tendo hilo linazidi kuwa ukumbusho mchungu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuzungumzia afya ya akili , suluhu za amani katika uhusiano ,na hitaji la kulinda maisha ya vijana wetu wanapojiandaa kwa mushtakabali wa taifa.


Reader's opinions
  1. Ilhan   On   May 14, 2026 at 8:33 am

    An awesome piece of narrative Journalism btw, very sad indeed, she had dreams and someine just took ot away like it meant nothing

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *



Current track

Title

Artist

Background