SHA Yaongeza Bima ya Saratani na Wajawazito Kupata Huduma Bure
Written by Eunice Onyancha on May 14, 2026
Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) imetangaza kifurushi kipya cha huduma za afya cha mwaka 2026 kitakachowanufaisha zaidi wagonjwa wa saratani na kina mama wajawazito kufuatia agizo la Rais William Ruto.
Katika maboresho hayo, fedha za matibabu ya saratani zimeongezwa kutoka Sh550,000 hadi Sh800,000 kwa mwaka kwa kila familia ili kusaidia wagonjwa kupata huduma za chemotherapy na radiotherapy bila changamoto za kifedha.
Wakati huo huo, mpango wa Linda Mama umeboreshwa na kuwa “Linda Jamii,” ambapo kina mama wajawazito sasa watapata huduma za uzazi bila malipo katika vituo vya afya vya ngazi ya pili na ya tatu. Huduma hizo zitajumuisha kujifungua kawaida au kwa upasuaji, kliniki za kabla na baada ya kujifungua, pamoja na dawa na vipimo vya maabara.
Waziri wa Afya Aden Duale alisema hatua hiyo inalenga kuhakikisha Wakenya wote wanapata huduma bora za afya bila kubebeshwa mzigo mkubwa wa gharama.
Agizo la Rais Ruto na Marekebisho ya SHA.lililotolewa wakati wa hotuba ya Hali ya Taifa ya mwaka wa 2025 na kuthibitishwa mnamo Mei 2026, linakusudia kuimarisha utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote .”SHA sio bima tu, ni ulinzi wa kijamii. Hatutamwacha yeyote nyuma,” Rais Ruto alinukuliwa akisema.Kifurushi hiki kipya pia kimeongeza kiwango cha matibabu ya dharura na magonjwa sugu .
Aidha, SHA imeongeza kiwango cha huduma za magonjwa sugu na matibabu ya dharura hadi Sh400,000 ,huku Wakenya wakihimizwa kujisajili kupitia *147# ili kufurahia manufaa hayo mapya.
