THE C S OF THE IDEAL FRIENDSHIP:
Written by Daniel Masese on July 30, 2024
Tuesday, 30th.July.2024.
The C S Of The Ideal Friendship:
Urafiki kitu bora,
Urafiki kitu barabara Ja barabara Ja barabara za bara.
Urafiki kitu ghali,
Wala si ughali wa ugali.
Humpa mtu imara,
Sura nazo sera;
Fikra nazo fakra;
Sawa mithili ya sahani sako kwa bako nayo kawa;
Fadhili nayo mapenzi katika
Uhalisia wa hali halisi na halisa.
Walio nazo hekima nazo busara huishi ngarange za msonobari kando,
Katika hili.
Huwaweka watu pamoja,
Huwapa watu faraja,
Hawabaguki abadan kataan bukrata wa ashiya!
Japo makabila ainati.
Msena siku akija,
Kumwacha usikubali katu!
Banana naye mithili ya ruba ngozini pa hayawani mbugani.
Matatizo ndicho cheti maridhawa cha kuudhihirisha dhahiri shahiri mithili ya thurea za nyota angani:
Ubinadamu, ukarimu, usena nao utu wa dhati si wa chati.
Aidha: huyadhihirisha mapenzi, fadhila, huruma pamwe nao wema.
What are The C S Of The Ideal Friendship?
By Professor and Philosopher Daniel Masese.