Leadership

Written by on June 3, 2026

Kila mtu anaweza kuwa msimulizi wa hadithi. Sote tunauwezo wa kusimulia hadithi zinazoguza mioyo ya
timu zetu kuzitoa katika kulegea na kuwapa nguvu. “ikiwa wewe ni kiongozi ni lazima uwe msimulizi wa
hadithi.” Daima tumekuwa tukisimulia hadithi ili kuelewa ulimwengu unaotuzunguka, mazingira
tunayoishi na muhimu zaidi kujielewa sisi wenyewe.
Kwenye makala haya nitakufunza jinsi ya kutumia simulizi sahihi kulingana na wakati ambao timu yako
inapitia na lengo unalolifuata. Kabla ya kusimulia hadithi yafaa ujiulize maswali kadhaa.
 Timu yako ina nafasi gani katika hii hadithi?
 Ni nini kinachozuia mafanikio yenu?
 Maono yako yamafanikio ni yapi?
 Ni hamu gani ya msingi itakayoifanya timu isongee kuelekea lengo la pamoja?
 Ni mabadiliko yapi ya kibinafsi yanayohitajika.
Simulizi saba za nadharia ya “CHRISTOPHER BOOKER”Mwandishi wa The Seven Basic Plots inatambua
miundo ya msingi ya hadithi ambazo zimetumika sana kwa maelfu ya miaka na unapoitumia ukitoa
hotuba zako utakuwa kiongozi mwenye nguvu na mwenye ushawishi mkubwa. Hivi ndivyo unaweza
kutumia ploti hizi katika uongozi.
1. Overcoming the monster [Kushinda jini]: Itumie unapohamasisha timu yako kukabiliana
na changamoto. Unawaonyesha kuwa adui ni mkubw lakini mna uwezo wa kumshinda.
2. Rags to Riches [Kutoka chini hadi juu]: Inafaa sana kwa ajili ya kujenga matumaini.
Unasimulia hadithi ya kampuni au mtu aliyeanza bila kiyu na sasa amefanikiwa ili
kuonyesha kuwa uvumilivu unalipa.
3. The quest [Safari ya kutafuta]:Tumia hii kuelezea vision ya muda mrefu. Safari ni ndefu
na ina vikwazo lakini lengo kuu ni la thamani kwa kila mmoja.
4. Voyage and Return [Safari na Kurudi]:Inafaa unapotaka kuhimiza uvumbuzi [innovation].
Unatuma timu yako “uwanja mgeni” kujifunza vitu vipya kisha wanarudi na maarifa
yatakayobadilisha shirika.
5. Rebirth [kuzaliwa upya]: Inafaa Wakati wa mabadiliko makubwa ya kitasisi. Unakubali
kuwa njia za zamani hazifanyi kazi tena na ni Wakati wa shirika kuzaliwa upya.
6. Tragedy [Tukio la kuhuzunisha]:Itumie kama onyo. Unasimulia hadithi za kampuni
zilizofeli kwa sababu ya kiburi au kukataa kubadilika ili timu yako iepuke makossa hayo.
7. Comedy: Katika uongozi hii inahusu kutatua migogoro na kuleta maelewano pale
panapokuwa na mkanganyiko wa mawasiliano kati ya idara au watu.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *



Current track

Title

Artist

Background