Hadithi ya Ibrahimu

Written by on June 3, 2026

Jana usiku nimekuwa nikisoma bibilia kuhusu hadithi ya Ibrahimu alivyoagizwa kumtoa
mwanawe Isaka kama dhabihu. Hii ni hadithi ambayo nimekuwa nikisoma mara kwa mara ila
nikiiihadithia kwa marafiki, watoto au yeyote yule ninaielewa kwa njia nyingine tofauti. Je hili
limewai kutokea? Gafla unapata kitu kingine ambacho haukukitarajia. Hivyo ndivyo ilivyotokea
wakati wa Ibrahimu na Isaka.
Katika agano la kale Mungu aliwapenda wanawe sana ndiposa alikubali waweke dhambi zao juu
ya kondoo mkamilifu ili kondoo yule afe badala yao ndio sababu Yesu akaja akawa
mwanakondoo na hiki ndicho tuna pata Ibrahimu na Isaka wakikifanya asubuhi hiyo
alivyoamriwa na Mungu.
Katika kitabu cha mwanzo 22 Ibrahimu na Isaka wanakwea mlimani pamoja na wajakazi wake
ilikutoa dhabihu kwa sababu ya dhambi zao na Mungu wakati huu anamuamuru Ibrahimu
kumtoa mwanawe Isaka kama dhabihu.
Ilikuonyesha utiifu Ibrahimu aliongoza safari ya kwenda mlimani akijua vyema kuwa anaenda
kumtoa mwanawe kama dhabihu. Wee hii ni kazi ngumu ya kumpa mzazi kama nifikiriavyo
mimi najua unafikiria hivyo pia. Kwa mawazo yangu nafikiria Ibrahimu alikuwa na wakati
mzito wa kufikiria hata hivyo alimwamini mungu na akafanya jinsi alivyoambiwa afanye.
Ibrahimu alitwaa moto mkononi mwake na Isaka akiwa amebeba kuni walikwea mlima ule ila
Isaka akamuuliza babaye kuwa kondoo wa kumtoa sadaka yuko wapi? Kama mzazi
anayempenda mwanawe siwezi hata kuelezea uchungu aliokuwa nao Ibrahimu wakati huo.
Ibrahimu alimtazama Isaka na kumhakikishia kuwa Mungu ataleta dhabihu ambayo tutaitumia.
Ushaifikiria huzuni aliokuwa nao Ibrahimu?
Walipofika kilele cha mlima walijenga madhabahu na akamlaza Isaka juu ya madhabahu hayo
akiwa amemfunga kwa Kamba. Ibrahimu aliunyanyua mkono wake tayari kumtoa Isaka sadaka.
Baada ya kumaliza kusoma hadithi hii nilijaribu kulinganisha hadithi hii ya Isaka na Yesu na
nikapata kwamba wanafanana kwa njia kadhaa.
 Isaka alibeba kuni kuelekea mlimani . Yesu alibeba msalaba kuelekea mlimani.
 Isaka alilazwa juu ya kuni zilizokuwa juu ya madhabahu . Yesu alitundikwa
msalabani.
 Isaka alikuwa mtiifu kwa babake. Yesu pia hakukataa hata alipoomba kwenye
bustani ya Gethsemane.
 Wote walinyenyekea hadi walipofika madhabahuni.
 Isaka hakukataa kwa sababu alimwaminia babake . Yesu pia vivyo hivyo
Hata hivyo wao pia wanautofauti mwingi sana nayo ni :
 Ingawa wote walili waliongozwa kama kondoo wa dhabihu, Mungu alimwokoa
mwana wa Ibrahimu lakini Yesu hakuokolewa.
 Isaka alitolewa kama jaribu la Imani ila Yesu alitolewa kama mpango wa
ukomboozi.
 Isaka alinusurika kifo ila Yesu alikufa na akafufuka tena.
Vitu vyote walivyofanya Ibrahimu, Isaka na Yesu inaonyesha wazi kuwa walimuamini Mungu.
Kupitia kuamini kwao wote walibarikiwa na kumbuka hili lilisababisha Ibrahimu kubarikiwa
kote.
Kwa hivyo aslimia ngapi yako unaamini Mungu nayo? Na unaamini asilimia uliyompea
itakufikisha umbali upi? Kumbuka utiifu wako na uaminifu wako kwake ndio utasababisha
ubarikiwe kwa ukubwa.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *



Current track

Title

Artist

Background