NEEMA YA MABILIONI YA RAIS RUTO KAUNTI YA NYAMIRA
Written by RadioVuna on June 3, 2026
Kwa miaka mingi kaunti ya Nyamira imezoeleka kwa utulivu wa shughuli za kilimo na biashara
ndogondogo hata hivyo Aprili 13, 2026 jua la asubuhi lilipochomoza lilichomoza na mwangaza wa
kipekee uliopasua ukimya huo kwa kishindo cha matumaini mapya. Ziara ya rais William Ruto katika
kaunti ya Nyamira haikuwa tu ya salamu za kisiasa bali salamu ya mabadiliko makubwa kupitia mfululizo
wa ahadi za miradi ya mabilioni ya pesa ambayo sasa inadhibitisha msemo wa kale “kucha mpya, mambo
mapya.”
Kama kweli elimu ni kioo cha jamii rais William Ruto alitoa kima cha Shilingi milioni 800 kwa sababu ya
ujenzi wa chuo kikuu cha Nyamira [Nyamira University College]. Milioni 500 kwa ujenzi wa majengo ya
masomo na milioni 300 kwa ujenzi wa hosteli. Milioni 500 kwa ujenzi wa hosteli za TVET na ufadhili
Zaidi kwa madarasa na hosteli katika chuo cha KMTC Nyamira.
Afya bora ni msingi wa maendeleo hivyo basi hospitali ya rufaa ya Nyamira ilipokezwa ahadi ya kima
cha shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya kuimarisha hospitali hiyo kwa ushirikiano na wafadhili kutoka Italia.
Licha ya kauti ya Nyamira kuwa na vipaji vingi, basi Vipaji bila uwanja ni mbegu kwenye mwamba
uwanja wa kisasa wa kima cha shilingi milioni 900 unajegwa ilikwamba wenye vipaji wafaidi Zaidi.
Fursa kwa vijana ni ujenzi wa taifa, mpango wa kujenga nyumba 10,000 za bei nafuu huko sironga, ujenzi
wa masoko ya kisasa kama Ikonge kwa kima cha shilingi milioni 70 na Magwagwa kwa shilingi milioni
200 pamoja na ujenzi wa eneo la viwanda kwa shilingi milioni 750 kwa ushirikiano na serikali ya kauti ni
kuleta ajira kwa vijana.
Miundombinu na usafiri pia haikubaki nyuma. Ahadi ya shilingi Milioni 300 kwa ujenzi wa kituo cha reli
Ikonge [Standard Gauge Railway] kwa ajili ya abiria na mizigo. Barabara ya Chebera-NyamusiNyamaiya
kwa shilingi Bilioni 3 na shilingi Bilioni 4.5 kwa barabara ya Tombe –isinta.
Mwisho mradi wa maji wa Bonyuyu uliahidiwa shilingi Bilioni 6.5 ilikuufanikisha kwani maji ni uhai.
Ndiposa miradi hii yote iwafaidi wakaazi wa Nyamira umeme unahitajiwa [last mile connectivity]
ulifaidika kupata shilingi milioni 900 ilikusaidia kote.
