Ugonjwa wa PERIPHERAL EDEMA.
Written by RadioVuna on June 3, 2026
Udadisi ndio mwanzo wa maarifa na katika kazi yangu ya udadisi nilibaini kati ya wapitanjia
kadhaa mmoja kati yao anatatizo la uvimbe haswa uvimbe kwenye mguu mmoja au miguu yote
katika kaunti ya Kisii ni kawa na hamu ya kufahamu chanzo cha tatizo hili ambalo nimeliona
kwa watu kadhaa. Kupitia utafiti wa kina nilioufanya nilibaini kuwa ugojwa huu unaitwa
PERIPHERAL EDEMA.
Nikawa na maswali kadhaa kichwani.Ila jibu ndilo hili kiganjani mwangu. Kisii inajulikana
kuwa na baridi lakini karibuni kumekuwa na ongezeko la joto kwa asilimia 30°C [86°F].
Ongezeko hili la joto linasababisha kutanuka kwa mishipa ya damu ili kupoza mwili hali ambayo
inasababisha majimaji kuvuja kutoka kwenye mishipa na kuingia kwenye tishu zizungukazo
mwilini. Maji haya huteremka chini kutokana na mvuto na kusababisha miguu na kifundo cha
mguu kuvimba. Pili upungufu wa protini aina ya albumin ambayo husaidia kuweka majimaji
ndani ya mishipa ya damu na inapopungua majimaji huvuja na kusababisha uvimbe. Mwisho,
utafiti wa tatu nilipata kwamba matatizo ya figo pia ni chanzo, hapa ni pale mwili unapopambana
na maambukizi ya mara kwa mara, figo zinaweza kushidwa kutoa chumvi na maji ya ziada
mwilini na hili husababisha uvimbe. Basi ni vyema tufahamu ugonjwa huu wa PERIPHERAL
EDEMA.
Peripheral Edema
Huu ni uvimbe unaotokana na maji ambayo mara nyingi hutokea kwa miguu, vifundi vya miguu
na mikono pia unaweza kuathiri uso na tumbo. Hali hii mara nyingi hufanya sehemu ya mwili
kuvimba kwa sababu maji mengi yamenaswa ndani ya tishu za mwili.
Aina
Uvimbe wa gafla [Acute Peripheral Edema]: hutokea ndani ya saa 72 mara nyingi baada
ya jeraha.
Uvimbe sugu [Chronic Peripheral Edena] : Husababishwa na damu kushidwa kurudisha
damu vizuri {venous insufficiency}
Drug-induce edema : Husababishwa na athaari ya dawa Fulani kama ya shinikizo la
damu au steroids.
Idiopathic Edema : Hii mara nyingi huwapata wanawake kabla ya kukatika kwa hedhi.
Dalili
Sehemu za mwili kuonekana zimevimba.
Ngozi kuonekana nyororo na ambayo imebadilisha rangi.
Maumivu katika eneo lililovimba.
Kuongezeka kwa uzito kutokana na maji yaliyotuama mwilini.
Vyanzo vya kawaida
Kukaa au kusimama kwa mda mrefu.
Ujauzito
Kula chumvi nyingi
Athiri za dawa Fulani
Magojwa kama kufeli kwa moyo au figo
Kinga na matibabu
Kupunguza chumvi tunayoila.
Mazoezi ya kutembea kidogo.
Compression socks ilikusaidia kusukuma maji yasituame.
Dawa za kutoa maji [Diuretics] ambazo husaidia kutoa maji ya ziada kupitia mkojo.
Wakati wa kumwoma daktari
Uvimbe unapotokea bila sababu ya jeraha.
Upungufu wa pumzi au maumivu ya kifua.
Uvimbe wa mguu mmoja tu [hii inaweza kuwa ishara ya damu kuganda]
Una maumivu makali sana.
Madhara ya uvimbe usipotibiwa
Uharibifu wa kudumu wa tishu.
Maambukizi ya vidonda vya Ngozi. [Cellulitis]
Mzunguko mbaya wa damu. [Deep vein thrombosis]
Kupungua kwa uwezo wa kutembea.
Huenda umemwona mmoja au una mmoja ambaye ako na hali hii au tatizo hili ni vyema ufike
hospitalini ili uweze kupokea na jinsi gani utajisaidia iwapo utapatikana na tatizo hili la
Peripheral Edema.
