Historia ya ukiukaji wa usalama wa Marais nchini Kenya inaonyesha mabadiliko makubwa

Written by on May 25, 2026

Historia ya ukiukaji wa usalama wa Marais nchini Kenya inaonyesha mabadiliko makubwa kutoka kwa mapinduzi ya kisiasa hadi raia wanaovamia majukwaa kuomba usaidizi, na sio kwamba mchezo huu ulianza juzi bali ulianza kuanzia kwa Rais wa kwanza nchini Kenya Rais Jomo Kenyatta.

Mnamo Oktoba 25, 1969 wakati wa ghasia zilizoshuhudiwa katika kaunti ya Kisumu, mawe yalirushawa Wakati Rais Jomo Kenyatta akitoa hotuba na hili liliwalazimu maafisa wa polisi kufwatua risasi ili kusafisha njia.

Agosti mwaka 2004 Rais Mwai Kibaki alirukiwa na kijana mmoja katika kaunti ya Mombasa alipokuwa akitoa hotuba jukwaani. Ilisemekana kwamba mwanamume huyo aliyekwa amechanganyikiwa aliruka vizuizi na kumshika rais mkono jukwaani.

Rais wa nne Uhuru Kenyatta pia alipitia mkondo huo huo. Katika mwezi wa Machi na Juni mwaka 2021 matukio matatu mtawalia yalifanyika. Msafara wa rais eneo la Muthaiga ulizuiliwa, kijana mmoja alijaribu kumkaribia huko Lamu na kijana aliyekimbia kwa zulia jekundu la Rais mbila viatu katika kaunti ya Kisumu.

Masaibu haya bado yanazidi kukua makubwa kila kuchao. Rais William Ruto masaibu haya yamekuwa yakimwandama moja baada ya lingine. Mei 4, 2025 kijana mmoja barubaru alirusha kiatu kuelekea jukwani huko Migori lakini kikamkosa Ruto.Februari 2026 watu wawili tofauti walikimbilia jukwaa la Rais katika mikutano ya Mombasa na Wajir. Mei 24, 2026 kijana aliyeshika Bibilia alipanda jikwaani Ganze Kilifi kaunti na kumshika Rais begani akiwa anhutubia.

Pengine waweza kujiuliza iwapo kuna uhusiano wa mfumo wa matukio haya.

Motisha ya kiuchumi huonekana kama sababu kubwa zaidi tofauti na miaka ya awali ambapo ambapo yalikuwa mapambano ya nguvu za kisiasa. Uvamizi huu wote wa kuanzia mwaka wa 2004 unahusisha raia masikini wanaotafuta pesa au kazi kutoka kwa rais. Maeneo ya pwani yanaongoza kwa matukio haya kwa sababu mikutano ya hadhara ya nje hulegeza udhibiti wa umati.

JE HII TUIITE “WIMBI LA KUIGANA [copycat effect]  AMA?


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *



Current track

Title

Artist

Background