Mshukiwa aliyetoroka korokoroni akamatwa
Written by Edgar Ombati on June 3, 2026
Mshukiwa mkuu wa mauaji yake Meshack Mainye,ametiwa mbaroni hatimaye baada ya kutoroka korokoroni.
Mshukiwa huyo alitoroka kutoka kituo Cha polisi Cha Sengera,Manga kaunti ya Nyamira.
Jeferstone Mokaya mwenye umri wa miaka 27 anashukiwa kumvamia na kumuua mjomba wake ,mwezi Oktoba mwaka Jana,kabla ya kuuzika mwili wake kwenye shamba la mahindi,kijijini Nyamwaya eneo bunge la kitutu masaba kaunti ya Nyamira.
Hakimu Briana Otieno ameamuru mshukiwa huyo kuzuiliwa katika kituo Cha polisi Cha Nyamira kwa siku kumi zaidi ili kuruhusu uchunguzi kukamilishwa kabla ya mshukiwa kurejeshwa mahakamani tarehe kumi na Moja kujibu mashtaka.
