WAKULIMA WA MIWA OLONTARI WAANDAMANA
Written by Obwoge Joseph on May 23, 2023

Magurudumu yachomwa nje ya kampani ya Sukari ya Mara: PICHA KWA HISANI
Mwandishi: Whitney Akunga
Hali ya wasi wasi imegubika kampuni ya Sukari ya Mara tawi la Olontari baada ya wakulima wa miwa kumfungia ofisini meneja wa daraja la uzani wa kampuni hiyo John Richardson.
Wakulima walioandamano hadi ofisini mwake wamemlaumu meneja huyo kwa kuwafuta kazi zaidi ya wafanyikazi 30 kwa njia tatanishi.
Waandamanaji hao waliokuwa na ghadhabu kubwa walifunga lango kuu la kampuni hiyo na kuwasha moto barabarani, hali iliyosababisha kutatizwa kwa shughuli za kawaida.
Mmoja wa waandamanaji alikuwa na haya ya kusema,“Meneja wa eneo hili Bwana Richardson amepewana nyaraka nyngi za kusitishwa kazi ya wafanyakazi, kwa zaidi ya watu 25 na sasa wenyeji wa eneo hili wameamua kwamba lazima meneja huyu aende la sivyo hakuna shughuli itaendelea katika kiwanda hiki”.
Wakati wa maandamano hayo, trakta zinazihudumu katika kampuni hiyo zililazimika kuegeshwa kando ya barabara, na kulemaza operasheni za kiwanda hicho cha sukari.
Maji yalipozidi unga, maafisa wa polisi walifika ili kumwokoa meneja aliyejifungia ndani ya ofisi na kutuliza hali hiyo tete.
Wakulima hao sasa wamemuomba waziri wa kilimo Peter Munya, kusuluhisha mgogoro uliopo kati ya wakulima na usimamizi wa kampuni hiyo.
