WANAWAKE 7 HUFA KILA SIKU NCHINI KENYA KUTOKANA NA UAVYAJI MIMBA

Written by on September 29, 2022

Eznahs Nyaramba of Young Women Democrats  PHOTO: Vuna Media

Kifuatia ongezeko la visa vya uayvaji mimba vinavyoripotiwa kila mwaka nchini Kenya, kwa asilimia ishirini (20%), (mwaka wa elfu mbili ishirini na moja 29%, mwaka wa elfu mbili ishirini na mbili 49%), wazazi wameombwa kuwashauri wanao kujilinda kutokana na mimba za mapema.

Kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Diniani (WHO), wasichana na wanawake wengi wanaendelea kufa na kukabiliwa na matokeo mabaya ya uavyaji mimba usio salama, hata hivyo kuna ukosefu wa taarifa kuhusu jinsi ya huduma bora inaweza kutolewa kwa wasichana na wanawake wenye matatizo yanayohusiana na uavyaji mimba.

Mkurugenzi mkuu wa Chama cha kutetea maslahi ya kina mama na wasichana Kisii cha ‘Young Women Democracts’ Aznahs Nyaramba amewaonya baadhi ya wauguzi dhidi ya kuwasaidia kina mama  pamoja na wasichana kuafya mimba.

”Tattizo kubwa Kisii kwa baadhi ya wasichana na akina mama wetu ni kuogopa mimba za mapema ilhali hawaogopi ugonjwa wa Ukimwi,” ameeleza Eznahs.Eznahs

Vile Vile amewakashifu vikali baadhi ya wauguzi  wenye mazoea ya kuendeleza uavyaji mimba, na kusisitiza kwamba atahakikisha wauguzi hao watachukulia hatua kali kulingana na sheria.

”Madaktari wetu mmependa pesa sana kuliko maisha ya akina mama wetu, msichana akipata mimba mwaache ajifungue ajipe mafunzo yeye mwenyewe, kuwa kielelezo bora, wape mafunzo jinsi ya kuwalinda na kuwatunza watoto wao vwema,” ameeleza Aznahs.

Amewashauri kuwa endapo  mama au msichana atakuwa na tatizo la  kuhatarisha maisha yake kutokana na mimba, watafute suluhu kutoka kwa daktari aliye na ujuzi  wa hali hiyo amshugulikie  hili kuokoa maisha yake.

Haya yanajiri wakati Kenya imejumuika na mataifa mengine duniani kusherehekea na kuidhinisha siku ya uavyaji mimba salama.

 

 


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *



Current track

Title

Artist

Background