MZOZO CHAMANI UDA -Ripoti na John M.

Written by on July 22, 2021

                       

 Mzozo mpya  wa umilikaji wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) unatokota chamani baina ya mwenye kiti wa awali Mohamed Abdi Noor na aliyekua senator Johnstone Muthama, , Boni Khalwale  na katibu mkuu wa chama hicho Veronica Maina. Chama hiki kinaaminika kuendeshwa na Naibu wa rais Dkt William Ruto.

Watatu hawa ambao ni wandani wa naibu rais, wamepeleka malalmishi yao kwa msajili na mtatuzi wa mizozo ya vyama vya kisiasa.Katika harakati ya kupata suluhu la umiliki hasa wa chama hicho.

Kwa mujibu wan akala zilizo wakilishwa mbele ya kamati hiyo, Noor anadai kuwa Muthama na Maina kwa kutwaa uongozi wa chama bila ya kuzingatia katiba ya chama hicho.Noor anataka kamati hiyo kubatili mabadiliko hayo yanayo mpa Muthana uwezo wa kuwaMwenyekiti na kumruhusu yeye kuendelea kuhudumu kama mwenyekiti halali wa chama.

Katika  ujumbe wake uliowasilishwa Noor alisema“I am aware on my own knowledge that the Registrar of Political Parties unlawfully made changes to the party’s National Executive Council (NEC) officials through Gazette Notice No. 1233 dated January 29, 2021, and 2739 published on March 19, 2021.”Wasilisho lake la Julai 12, 2021lilizidi kusema kuwa: “The Registrar deliberately ignored complaints and reservations leading to the change of officials.”

Anasema kuwa katibu mkuu aliyeng’atuliwa mamlakani Bw. Mohamed Sahal aliitisha mkutano mnamo Disemba 11, mwaka jana,ambapo fomu za PP10 zilisainiwa na maafisa ilikubadili jina la chama kutoka Party for Development and Reforms (PDR) kwenda UDA, lililo kubalika na wote na baadaye kuonekana walitumika kufanya mabadiliko chamani

Mabadiliko haya,yamekuja juma moja tu baada UDA kunyakua kiti cha ubunge cha kwanza pale Kiambaa katika uchaguzi mdogo uliokamilika juzi na kuonyesha ubabe wa kisiasa Mlima Kenya kati ya Rais na naibu wake

Akisherehekea ushundi huo wa kiambaa Dkt Ruto alisema kuwa,“ni wazi kuwa ushindi wa UDA unaonyesha kuwa watu wa Kiambaa walichagua kesho (UDA) dhidi ya  jana (Jubilee)”.Kuongea kuhusu za mwaka ujao Ruto ameonekana akisema kuwa kitakuwa chama chake cha ugombea katika uchaguzi mkuu wa 2022.

Akiwasilisha malalamishi mbele ya kamati ya kutatua mizozo ya kisiasa na vyama, Noor ameorodhesha kamati hiyo na chama cha UDA kama watakao hojiwa.

Noor anashikilia kuwamabadiliko yaliyofanywa hayakuchukua mkondo halisi kisheria hata kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali ili kuruhusu wote kushiriki hivyo kuwapa wachache nafasi,hivyo kutaka mahaka kumkosesha msajili wa vyama na husika akiwemo Bw.Sahal ambaye kama katibu alikuwa mtumishi wa serikali kinyume na sheria ya vyama. Kesi hii inatarajiwa kutajwa tena Julai 28,2021, wakati mahakama itatoa mwelekeo.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *



Continue reading

Current track

Title

Artist

Background