MTAALA WA CBC KATIKA NJIA PANDA

Written by on September 16, 2022

Mtaala mpya wa elimu nchini unaendelea kuzua gumzo miongoni mwa wakenya ambao wamegubikwa na hali ya sintofahamu, iwapo mtaala huo uondolewe, usalie au ufanyiwe marekebisho.

 

Ikumbukwe nyakati za kempeni umoja wa Kenya Kwanza uliahidi kuutupilia mbali mtaala huo ikiwa wangechaguliwa.

 

Na sasa yote ni bayana kwamba mrengo huo umeshika hatamu ya uongozi, kulingana na rais William Ruto wakenya watashirikishwa kikamilifu katika mfumo huo mpya ili tathmini itowele iwapo atauendelea ama kukataliwa.

 

Waziri wa elimu anayeondoka mamlakani Profesa George Magogha ameweka bayana kurithika kwake na mfumo huo baada ya kutalii, kukagua na kufungua rasmi baadhi majengo yatakayotumiwa kuuendeleza mfumo huo wa masomo.

 

Mtaala huu wa CBC ni kati ya miradi iliyoanzishwa na wizara ya elimu chini ya uongozi wake rais mstaafu Uhuru Kenyatta a iwapo utaendelea, itakumbukwa katika historia ya Kenya kuwa kati ya mafanikio ya serikali yake.

 

Linalosalia kwa sasa ni swali litakalojibiwa na wakenya, iwapo mfumo huo utandelea au kutupiliwa mbali.

 


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist

Background